925- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Wenye huruma wanahurumiwa na Mwingi wa huruma (Tabaarak wa Ta´ala). Wahurumieni waliyoko ardhini atakuhurumieni aliyeko juu ya mbingu.”
Ameipokea Abu Daawuud (4941), at-Tirmidhiy (1/350), Ahmad (2/160), al-Humaydiy (591), kupitia kwake al-Bukhaariy katika ”at-Taariykh” (64/574), Ibn Abiy Shaybah (8/526), al-Haakim (4/159) ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye, al-Khatwiyb katika ”Taariykh Baghdaad” (3/260), al-Bayhaqiy katika ”Shu´b-ul-Iymaan” (7/476) na Abul-Fath al-Khiraqiy katika ”al-Fawaa-id al-Multaqatah” (222-223) kupitia kwa Sufyaan bin ´Uyaynah, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka Abu Qaabuus, mtumwa wa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”
al-Khiraaqiy ameisahihisha na Ibn Hajar anaona kuwa ni yenye nguvu kwa sababu ameinyamazia katika ”Fath-ul-Baariy”[1].
Faida:
Neno في السماء maana yake ni juu ya mbingu ni kama mfano wa Allaah (Ta´ala) pale aliposema:
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ بَدَأَ الْخَلْقَ
“Sema: “Tembeeni juu ya ardhi na mtazame jinsi [Allaah] alivyoanzisha uumbaji.”[2]
Hadiyth ni moja katika dalili nyingi zinazothibitisha kwamba Allaah yuko juu ya viumbe vyote. Haafidhw adh-Dhahabiy ametunga kitabu ”al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar” juu ya maudhui hayo. Nakaribia kumaliza ufupisho wake. Nimekiwekea utangulizi wake, kuonyesha vyanzo vya Hadiyth na kuzipa hukumu pamoja na kuondosha ndani yake mapokezi yote dhaifu.
[1] 10/440.
[2] 29:20
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (2/596)
- Imechapishwa: 11/05/2019
925- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Wenye huruma wanahurumiwa na Mwingi wa huruma (Tabaarak wa Ta´ala). Wahurumieni waliyoko ardhini atakuhurumieni aliyeko juu ya mbingu.”
Ameipokea Abu Daawuud (4941), at-Tirmidhiy (1/350), Ahmad (2/160), al-Humaydiy (591), kupitia kwake al-Bukhaariy katika ”at-Taariykh” (64/574), Ibn Abiy Shaybah (8/526), al-Haakim (4/159) ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye, al-Khatwiyb katika ”Taariykh Baghdaad” (3/260), al-Bayhaqiy katika ”Shu´b-ul-Iymaan” (7/476) na Abul-Fath al-Khiraqiy katika ”al-Fawaa-id al-Multaqatah” (222-223) kupitia kwa Sufyaan bin ´Uyaynah, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka Abu Qaabuus, mtumwa wa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”
al-Khiraaqiy ameisahihisha na Ibn Hajar anaona kuwa ni yenye nguvu kwa sababu ameinyamazia katika ”Fath-ul-Baariy”[1].
Faida:
Neno في السماء maana yake ni juu ya mbingu ni kama mfano wa Allaah (Ta´ala) pale aliposema:
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ بَدَأَ الْخَلْقَ
“Sema: “Tembeeni juu ya ardhi na mtazame jinsi [Allaah] alivyoanzisha uumbaji.”[2]
Hadiyth ni moja katika dalili nyingi zinazothibitisha kwamba Allaah yuko juu ya viumbe vyote. Haafidhw adh-Dhahabiy ametunga kitabu ”al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar” juu ya maudhui hayo. Nakaribia kumaliza ufupisho wake. Nimekiwekea utangulizi wake, kuonyesha vyanzo vya Hadiyth na kuzipa hukumu pamoja na kuondosha ndani yake mapokezi yote dhaifu.
[1] 10/440.
[2] 29:20
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (2/596)
Imechapishwa: 11/05/2019
https://firqatunnajia.com/yule-aliye-juu-ya-mbingu-anawarehemu-wenye-huruma/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)