Swali: Je, ufukara unaingia katika aina za majaribio ya Allaah?

Jibu: Yote ni majaribio utajiri na umasikini. Huyu anapewa mtihani wa furaha, mwingine anapewa mtihani wa yenye kumdhuru, mwingine anapewa mtihani wa uzima, mwingine anapewa mtihani wa maradhi, mwingine anapewa mtihani wa utajiri na mwingine anapewa mtihani wa umasikini, mwingine anapewa mtihani wa kazi, mwingine anapewa mtihani wa kunyimwa kazi. Yote hayo ni majaribio na mtihani.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21608/هل-يدخل-الفقر-في-انواع-الابتلاء-من-الله
  • Imechapishwa: 28/08/2022