Swali: Matendo ni nguzo na sehemu ya imani au ni sharti ya kutimia kwake?

Jibu: Matendo ni sehemu ya imani. Haifai kusema kuwa ni sharti ya kutimia kwake. Matendo ni sehemu ya imani kama tulivyotangulia kusema. Imani ni kauli ya ulimi na kauli ya moyo, ´amali ya moyo na ´amali ya viungo kama tulivyoyangulia kusema. Kusema kuwa matendo ni kitu kilicho nje ya imani ni kauli ya Murji-ah. Murji-ah ndio wanasema kuwa matendo ni kitu kilicho nje ya imani. Wanasema vilevile matendo yanailazimu imani. Wanasema pia matendo yanapelekea katika imani. Wanasema pia kwamba matendo ni dalili ya imani au maneno yanayofanana na hayo. Yote haya ni katika maneno ya Murji-ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4735
  • Imechapishwa: 01/05/2015