Hatulijui jambo hili analouliza. Anauliza kuhusu kusoma Qur-aan kwa ajili ya wafu. Hili halina asili kabisa. Yule anayesoma Qur-aan kwa ajili ya maiti baada ya kufa, kaburini, juu ya jeneza au kaburini, yote haya hayana msingi. Kwa msemo mwingine kusoma Qur-aan kwa ajili ya wafu makaburini, wakati wa kumzika au katika usiku aliyofariki ambapo watu hukusanyika na kumsomea, yote haya hayana msingi. Hatulijui jambo hili kuwa na msingi wowote katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1023/حكم-قراءة-القران-على-الميت-بعد-الدفن