57Ulipowadia wakati wa Elizabeti kujifungua, alizaa mtoto mwanaume. 58Majirani zake na jamii zake wakasikia jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu, nao wakafurahi pamoja naye. 59 Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zekaria, ambalo ndilo jina la baba yake. 60Lakini mama yake akakataa na kusema: “Hapana! Jina lake ataitwa Yohana.” 61Wakamwambia: “Hakuna mtu yeyote katika jamaa yako mwenye jina kama hilo.” 62 Basi wakamfanyia Zekaria baba yake ishara ili kujua kwamba yeye angependa kumpa mtoto jina gani. 63Akaomba wampe kibao cha kuandikia na kwa mshangao wa kila mtu akaandika: “Jina lake ni Yohana.”

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Luka 01:57
  • Imechapishwa: 18/01/2020