Swali: Ni ipi tafsiri sahihi kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ

”Allaah ana wasifu wa juu kabisa.”[1]

Jibu: Maana yake ni wasifu wa juu kabisa ambaye hafanani na chochote:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[2]

Hakika Yeye (Ta´ala) ana sifa za juu kabisa, kwa msemo mwingine wasifu wa juu kabisa. Hakuna chochote mfano wake. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ni mkamilifu katika dhati, majina, sifa na matendo Yake.

[1] 16:60

[2] 42:11

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31203/ما-تفسير-قوله-تعالى-ولله-المثل-الاعلى
  • Imechapishwa: 16/10/2025