Yaa Siyn anasomewa anayetaka kukata roho, na si kwa maiti

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Suurah Yaa Siyn juu ya kaburi la maiti?

Jibu: Haisomwi chochote juu ya makaburi, si Yaa Siyn wala kitu kingine. Yaa Siyn inasomwa kwa yule aliye katika hali ya kukata roho kabla hajafariki. Inapendekezwa kusomwa kwa anayetaka kukata roho kabla hajafariki kutokana na Hadiyth iliyopokelewa juu ya hilo. Ama baada ya kuzikwa, makaburi hayasomewi Yaa Siyn wala kitu chochote wala hakuswaliwi hapo. Yote hayo ni Bid´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31695/ما-حكم-قراءة-سورة-يس-على-قبر-الميت
  • Imechapishwa: 15/11/2025