Wudhuu´ wa anayeacha kutaja jina la Allaah kabla yake

Swali: Mtu ametawadha pasi na kutaja jina la Allaah?

Jibu: Kutaja jina la Allaah wakati wa kutawadha ni wajibu. Yule aliyetawadha bila kulitaja kwa kusahau au kwa kutokuwa na ujuzi wa hukumu ya Shari´ah, basi wudhuu´ wake ni sahihi. Lakini yule aliyeacha kulitaja kwa makusudi, basi wudhuu´ wake ni batili kwa mujibu wa maoni yaliyo sahihi zaidi miongoni mwa maono ya wanazuoni. Hii ni kwa mujibu wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hana wudhuu´ yule ambaye hakutaja jina la Allaah kabla yake.”[1]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na Ibn Maajah kupitia njia nyingi za upokezi zinazopeana nguvu.

[1] Ahmad (04/418), Abu Daawuud (01) na Ibn Maajah (399).

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/203-204)
  • Imechapishwa: 31/10/2026