Du´aa ya kuosha kila kiungo cha wudhuu´ ni Bid´ah

Swali: Je, kuna du´aa yoyote iliyothibiti katika Shari´ah inayotamkwa wakati wa kutawadha?

Jibu: Haijathibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akisoma du´aa yoyote wakati wa kuosha au kupangusa viungo vya wudhuu´. Du´aa zinazotajwa kuwa zinasomwa wakati wa kuosha au kupangusa kila kiungo ni Bid´ah zisizo na msingi wowote. Kinachotambuliwa kwa mujibu wa Shari´ah ni kutaja jina la Allaah mwanzoni mwa wudhuu´, na kutamka shahadah mbili baada ya muadhini, kisha kusema:

اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين

“Ee Allaah! Nifanye kuwa miongoni mwa wenye kutubu na nifanye kuwa miongoni mwa wenye kujitwahirisha.”

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/205)
  • Imechapishwa: 31/10/2026