Swali: Je, maana ya kutia vidole katikati ya ndevu wakati wa wudhuu´ ni kwamba ni wajibu maji kufika kwenye ngozi iliyo chini ya ndevu?
Jibu: Ni wajibu kuosha sehemu ya nje ya ndevu nyingi, lakini si wajibu kuosha sehemu ya ndani ya ndevu hizo wala ngozi iliyo chini yake. Hata hivyo ni jambo limewekwa katika Shari´ah kupitisha vidole katikati ya ndevu ili maji yafike ndani yake. an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakuna tofauti ya maoni kuhusu wajibu wa kuosha sehemu ya nje ya ndevu nyingi na si wajibu kuosha sehemu ya ndani ya ndevu hizo wala ngozi iliyo chini yake kwa makubaliano ya wanazuoni. Haya ndio maoni ya wanazuoni wengi miongoni mwa Maswahabah, wanafunzi wao na wale waliokuja baada yao.”
Ibn Rushd amesema:
“Hili ni jambo ambalo sijui kwamba kuna tofauti yoyote ya maoni kuhusu hilo.”
Ama ikiwa ndevu ni chache kiasi kwamba ngozi ya chini yake inaonekana, basi ni wajibu kuosha sehemu ya ndani na sehemu ya nje ya ndevu hizo.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/206-207)
- Imechapishwa: 31/10/2026
Swali: Je, maana ya kutia vidole katikati ya ndevu wakati wa wudhuu´ ni kwamba ni wajibu maji kufika kwenye ngozi iliyo chini ya ndevu?
Jibu: Ni wajibu kuosha sehemu ya nje ya ndevu nyingi, lakini si wajibu kuosha sehemu ya ndani ya ndevu hizo wala ngozi iliyo chini yake. Hata hivyo ni jambo limewekwa katika Shari´ah kupitisha vidole katikati ya ndevu ili maji yafike ndani yake. an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakuna tofauti ya maoni kuhusu wajibu wa kuosha sehemu ya nje ya ndevu nyingi na si wajibu kuosha sehemu ya ndani ya ndevu hizo wala ngozi iliyo chini yake kwa makubaliano ya wanazuoni. Haya ndio maoni ya wanazuoni wengi miongoni mwa Maswahabah, wanafunzi wao na wale waliokuja baada yao.”
Ibn Rushd amesema:
“Hili ni jambo ambalo sijui kwamba kuna tofauti yoyote ya maoni kuhusu hilo.”
Ama ikiwa ndevu ni chache kiasi kwamba ngozi ya chini yake inaonekana, basi ni wajibu kuosha sehemu ya ndani na sehemu ya nje ya ndevu hizo.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/206-207)
Imechapishwa: 31/10/2026
https://firqatunnajia.com/ndevu-zinazopaswa-kuoshwa-ndani-na-nje/