Wudhuu´ wa ambaye tumboni mwake kuna mingurumo

Swali: Ikiwa mtu yuko katika hali ya wudhuu´, kisha akasikia sauti ya upepo tumboni mwake. Lakini upepo huo haukutoka kwenye tundu la haja kubwa. Ni ipi hukumu ya hilo? Je, ataendelea kuwa na wudhuu´ au wudhuu´ wake umechenguka?

Jibu: Ikiwa mtu yuko katika hali ya wudhuu´ na akasikia sauti ya upepo ndani ya tumbo lake, basi wudhuu´ wake hauharibiki kwa hilo ikiwa hakuna kitu kilichomtoka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu anapohisi kitu tumboni mwake, kisha akawa na shaka kwamba, je, kimetoka kwake kitu au hakikutoka, basi asiondoke msikitini mpaka asikie sauti au ahisi harufu.”[1]

Ameipokea Imaam Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

[1] Muslim (01/190).

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/256)
  • Imechapishwa: 08/11/2026