Ni sawa kupangusa juu ya kilemba ikiwa hakuna udhuru wowote?

Swali: Je, inajuzu kupangusa juu ya kilemba ikiwa hakuna udhuru, kwa maana si kwa sababu ya ugonjwa wala sababu nyingine, lakini mtu hataki kukivua kilemba chake na anapendelea kufuta juu yake?

Jibu: Mwenye kutawadha anaruhusiwa kupangusa juu ya sehemu ya kichwa na nywele zake zilizo wazi, kisha akakamilisha upangusaji juu ya kilemba chake, ikiwa alikivaa akiwa katika hali ya twahara. Mkaazi anaweza kufanya hivyo kwa muda wa mchana mmoja na usiku wake, na msafiri kwa muda wa michana mitatu pamoja na nyusiku zake, kama ilivyo katika ufutaji wa soksi za ngozi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivyo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/251)
  • Imechapishwa: 08/11/2026