Wudhuu´ wa ambaye ameweka plasta

Swali: Ni ipi hukumu ya plasta na inapasa kupanguswa wakati wa kuoga janaba? Je, inapasa kupanguswa wakati wa wudhuu´ ikiwa ipo juu ya kiungo cha wudhuu´?

Jibu: Ndiyo, plasta ikiwa imewekwa mgongoni, tumboni au sehemu nyingine na mtu anapaswa kuoga josho la janaba, basi inatosha kupitisha maji juu yake. Kwa maana kwamba maji yapite juu ya plasta hiyo na kufanya hivo inatosha. Ama ikiwa ipo kwenye sehemu za wudhuu´, kama mguu au mkono, basi inatosha kuipangusa juu yake. Ikiwa ipo kwenye mkono, anaipangusa wakati wa kuosha mkono. Ikiwa ipo usoni, anaipangusa wakati wa kuosha uso. Ikiwa ipo kwenye mguu, anapitisha maji juu yake na kuipangusa wakati wa kuosha mguu. Hii inatosha na haihitaji kufanya Tayammum pamoja nayo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3540/حكم-المسح-على-اللاصقة-في-الغسل-وفي-الوضوء
  • Imechapishwa: 10/09/2026