Urafiki na kafiri kwa ajili ya kuimarisha lugha yake ya kizungu

Swali: Je, inajuzu kufanya urafiki na waingereza au wamarekani ili kuimarisha lugha ya kingereza huku mtu akijilinda na dini yake?

Jibu: Hapana. Hata hivyo unaweza kuimarisha lugha kwa njia nyingine zisizo na kufanya urafiki na makafiri. Unaweza kuimarisha lugha kwa kuzungumza na ndugu zako waislamu wanaojua kingereza, kwa kurejea kanuni zake na kujifunza kwa wale wanaoifundisha ili uongeze ujuzi wako pale unapohitaji. Ikiwa huna haja nayo, basi hakuna sababu ya kujishughulisha sana nayo. Lakini ikiwa kuna haja, basi tumia njia salama kama kushirikiana na waislamu wanaoijua lugha hiyo. Huna haja ya kufanya urafiki na makafiri ili ujifunze kutoka kwao.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3527/حكم-مصادقة-الكفار-لاجل-تعلم-الانجليزية-منهم
  • Imechapishwa: 10/09/2026