Ana mwajiri kafiri ambaye anampenda kwa sababu ya kazi yake

Swali: Mimi nina mfanyakazi Mhindu na ninamfanya aniuzie. Ninamlisha chakula cha mchana na cha jioni, bali hata nacheka naye kwa sababu ni mfanyakazi mchangamfu. Je, hili linaingia katika kuwafanya makafiri kuwa marafiki (موالاة)?

Jibu: Ni wajibu kwako kuwaepusha, kutowaleta na uwabadilishe kwa waislamu. Huna haja wala dharurah ya kuwa na mfanyakazi mhindu, mkomunisti, mbuddha, mnaswara au mwingine yeyote. Allaah amekutosheleza kwa kuwepo waislamu. Kwa hivyo ni wajibu kwako kuwaepusha.

Ama kuhusu hili kuwa ni katika kuwafanya marafiki, hili linahitaji upambanuzi. Kuwaajiri kwao pekee hakuhesabiki kuwa ni kuwafanya marafiki, lakini haifai. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo. Ama kumfanya kuwa rafiki na mpendwa na kutangamana naye kama rafiki, hili ni aina ya kuwafanya marafiki. Kuwafanya marafiki ni tofauti na kuwasaidia (التولي): kuwafanya marafiki ni dhambi na kuwasaidia (ambako ni kule kuwaunga mkono dhidi ya waislamu) ni ukafiri. Kwa hiyo kuwafanya marafiki ni chini ya kuwasaidia: kuwafanya marafiki ni kuwapenda, kuwapa zawadi, kuwachekea au kuanza kuwapa salamu. Haya ni katika kuwafanya marafiki ambako ni haramu. Lakini kuwasaidia ni kuwasaidia dhidi ya waislamu na kuwapa nguvu juu ya waislamu, jambo ambalo ni kuritadi na ni katika mambo yanayobatilisha Uislamu. Tunajikinga kwa Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3529/حكم-معاملة-العامل-الكافر-معاملة-الصديق
  • Imechapishwa: 10/09/2026