Muislamu kuchangia pesa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa

Swali: Tulikuwa tunafanya kazi katika kampuni na mmiliki wake alikuwa mnaswara. Siku moja alituomba tutoe mchango wa fedha kwa ajili ya kujenga kanisa ambapo tukafanya hivyo. Ni yepi maoni yenu katika jambo hili?

Jibu: Hili ni jambo baya sana na halijuzu. Ni juu yao kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa hili ni ukafiri na kuritadi, kwa sababu ni kusaidia kusimamisha ukafiri. Kwa hiyo ni wajibu kwa aliyefanya jambo hili atubie kwa Allaah, arejee Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala), ajute, aache kabisa na asirudie tena jambo kama hili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3530/حكم-تبرع-المسلم-لبناء-كنيسة
  • Imechapishwa: 10/09/2026