Swali: Wakati ´Aaishah alipoulizwa ambapo akajibu: “Hulala kabla ya kuswali Witr.” Wakati mwingine hutanguliza Witr. Je, ndivyo?

Jibu: Hili ni katika baadhi ya nyusiku. Baadhi ya nyusiku anaswali Witr na nyusiku zingine anachelewesha Witr. Nilimuuliza juu ya zile nyusiku ambazo huchelewesha Witr… anachokusudia ni kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati fulani anaweza kulala kabla ya kuswali Witr. Amesema:

“Macho yangu hulala na moyo wangu haulali.”

Kwa maana ya kwamba huamka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili aswali Witr.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23815/%D9%87%D9%84-%D9%83%D8%A7%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D9%8A%D9%86%D8%A7%D9%85-%D9%82%D8%A8%D9%84-%D8%A7%D9%86-%D9%8A%D9%88%D8%AA%D8%B1
  • Imechapishwa: 06/05/2024