Swali: Leo kuna wanaosema kuwa tofauti katika mlango wa majina na sifa za Allaah sio jambo muhimu; ni mamoja ukathibitisha sifa miongoni mwa sifa au ukakanusha kwamba hilo halipelekei katika chochote katika hayo na akatoa mifano.

Jibu: Huyu yeye ndiye si muhimu. Huyu aliyesema hivi ndiye si muhimu. Mambo haya ni miongoni mwa mambo muhimu zaidi. Kwa sababu ni miongoni mwa misingi mikubwa ya dini na ya ´Aqiydah. Huyu anazungumza mambo asiyoyajua au anakusudia upotevu na tunaomba kinga kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17404
  • Imechapishwa: 07/12/2017