”Wewe ndiye uliyenisaidia baada ya Allaah”

Swali: Je, inajuzu kusema mfano wa maneno haya:

”Wewe ndiye ulonisaidia katika jambo fulani baada ya Allaah”?

Jibu: Hakuna tatizo kusema hivyo. Hapana vibaya kusema: ”Kama si kwa Allaah kisha wewe”, ”Hii ni kutoka kwa Allaah kisha kutoka kwako”. Kisichofaa ni kusema: ”Kama si kwa Allaah na wewe”, ”Hii ni kutoka kwa Allaah na kutoka kwako” au ”Alivyotaka Allaah na ukataka wewe”. Matamshi kama haya ndio hayajuzu, kwa msemo mwingine ”na” (الواو) haijuzu.

Lakini mtu akisema: ”Kama si kwa Allaah kisha wewe”, ”Alivyotaka Allaah kisha akataka fulani”, kwa sababu fulani alimsaidia au akasema: ”Wewe umenisaidia baada ya Allaah katika jambo fulani”, basi hilo halina tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1188/حكم-قول-انت-ساعدتني-في-كذا-بعد-الله
  • Imechapishwa: 06/02/2026