Swali 558: Nilimtajia Shaykh wetu maneno ya Abul-´Abbaas Ibn Taymiyyah:

“Sijui yeyote aliyepambanua kati ya talaka tatu zilizotolewa pamoja au zilizotenganishwa.”

Jibu: Nami sijui yeyote aliyesawazisha kati ya hizo.

Swali 559: Vipi ikiwa mtu atasema: “Wewe ni haramu kwangu na kwangu umeachika”?

Jibu: Ikiwa alikusudia kusisitiza jambo au kuzuia kitu, basi kuna kafara ya kiapo kwa mujibu wa wanazuoni waliotafiti suala hilo kwa kina.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 189
  • Imechapishwa: 11/03/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´