Weka pesa benki bila kuchukua faida

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka mali bila kuchukua faida juu yake kama amana au akaunti ya matumizi ya kawaida katika benki zilizopo sasa, pamoja na kuzingagia kwamba benki hizo zinashughulika na ribaa na kutoa faida?

Jibu: Haijuzu kuwapa mali waihifadhi kwao, kwa sababu wanashughulika na ribaa na hilo ni kuwasaidia katika ribaa. Lakini baadhi ya wanazuoni wamesema kwamba ikiwa ni kwa dharurah na hana mahali pa kuhifadhi mali yake na wala hakupata wa kuhifadhi mali yake isipokuwa kwa njia ya benki hizi, basi huenda ikajuzu kwa dharurah bila faida. Hata hivyo akijitahidi – Allaah akitaka – atapata mahali pa kuhifadhi mali yake, na asiwape benki hizi zinazotumia mali hiyo kuwasaidia katika ribaa na shari. Lakini kwa faida, hapana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1925/حكم-ايداع-المال-في-البنوك-الربوية-دون-اخذ-الفاىدة
  • Imechapishwa: 28/12/2025