Wazikaji kukanyaga juu ya kaburi wakati wa mchakato wa mazishi

Swali: Mtu anapozikwa na kufunikwa kwa udongo ni lazima kukanyaga juu ya kaburi kwa miguu au si lazima?

Jibu: Maiti anapozikwa, hapaswi kukanyagwa juu ya kaburi. Bali udongo unafunikwa kwa mikono, kisha maji yanamwagiwa juu ya kaburi na kuwekwa kokoto ndogo juu yake, halafu mtu aombwee msamaha na uthabiti. Hii ndiyo njia sahihi. Kaburi halipaswi kukanyagwa kwa mguu wala kukaliliwa juu yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiswali kuyaelekea makaburi na wala msikai juu yake.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kukaa mmoja wenu juu ya jiwe linalowaka moto mpaka liunguze ngozi yake ni bora kuliko kukaa juu ya kaburi.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1169/حكم-وطء-القبر-بالاقدام-اثناء-الدفن
  • Imechapishwa: 01/02/2026