Waumini watenda madhambi wataadhibiwa ndani ya kaburi?

Swali: Je, adhabu ya ndani ya kaburi inawahusu waumini watenda madhambi au ni kwa makafiri peke yao?

Jibu: Adhabu ya ndani ya kaburi yenye kuendelea inakuwa kwa mnafiki na kafiri. Kuhusu muumini mtenda madhambi anaweza pia kuadhibiwa ndani ya kaburi lake. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea katika “as-Swahiyh” zao kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita karibu na makaburi mawili na akasema: “Hakika wawili hawa wanaadhibiwa na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. Lakini hata hivyo ni jambo kubwa. Kuhusu mmoja wao alikuwa akitembea na kueneza umbea na mwengine alikuwa hajichungi na mkojo wake.”[1]

Tukio hili linatambulika ya kwamba wawili hawa walikuwa waislamu.

[1] al-Bukhaariy (218) na Muslim (292).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mjamuu´-ul-Fataawaa (17/434-435)
  • Imechapishwa: 29/05/2026