Mwanamke kuacha wazi nywele zake wakati wa adhaana

Swali: Je, ni haramu mwanamke kuacha nywele zake wazi wakati ambapo muadhini anaadhini na hakuna anayemuona isipokuwa wale ndugu zake wasioweza kumuoa na wanawake wenzake? Je, ni sahihi kwamba Malaika wanamlaani katika kile kipindi chote cha adhaana?

Jibu: Haya si sahihi. Inafaa kwa mwanamke kufunua nywele zake wakati muadhini yuko anaadhini, muhimu asionekane na mwanaume yeyote wa kando. Lakini anapotaka kuswali analazimika kufunika mwili wake mzima isipokuwa tu uso wake. Licha ya kwamba wanazuoni wengi wamemruhusu kuonyesha mikono yake pia. Hata hivyo salama zaidi ni yeye kufunika mikono pia. Hapa ni pale ambapo haswali mbele ya wanaume wa kando. Akiswali mbele yao basi analazimika kuufunika, kwa sababu haijuzu kwake kuonyesha uso wake isipokuwa mume na wale ndugu wasioweza kumuoa.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mjamuu´-ul-Fataawaa (12/202)
  • Imechapishwa: 29/05/2026