Swali: Baadhi ya waume pindi wanapoachana na wake zao wanachukua kila kitu walichowapa katika mahari na vyenginevyo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Mwanamke asipochagua mwanaume mwema, basi maisha yake yanakuwa ni mabalaa na matatizo kuanzia pale mwanzoni. Pengine hata mwanamke akajiua, kwa sababu hampendi mume wake. Aidha akapigwa na familia yake ili aweze kurudi kwa mume wake.

Asimwombe pesa yoyote. Asichukue chochote kutoka kwake, isipokuwa ikiwa mwanamke huyo anamchukia na yeye mwanaume bado anampenda. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha Thaabit bin Qays bin Shimaas (Radhiya Allaahu ´anh) kumtaliki mke wake na yeye mwanamke amrudishie shamba lake. Lakini ikiwa yeye mwanamke anampenda na yeye mwanaume anamchukia na pindi mwanamke anamsogelea basi anampiga, ili mwanaume apatae kusema kuwa anamchukia… Tunaishi katika kipindi cha matatizo. Mahakama zimejaaa matatizo ya kindoa. Sababu ni kuwa watu hawashikamani na Qur-aan na Sunnah.

Baba wenye tamaa wanawapiga wasichana zao na kuwatishia kipigo wakikataa kuolewa na waume fulani. Sambamba na hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asokuwa bikira asiozeshwe isipokuwa mpaka baada ya kutakwa ushauri wala bikira isipokuwa kwa idhini yake.” Wakasema: “Ni ipi idhini yake?” Akasema: “Kunyamaza kwake.”[1]

Sababu ni kama tulivosema tumeipa mgongo Qur-aan na Sunnah. Kwa ajili hiyo kumekuwa kuna matatizo mengi. Ikiwa umempa msikiti wote huu uliojaa dhahabu na ni wewe ndiye ambaye unamchukia, basi si halali kwako kuchukua chochote katika vile ulivyompa. Lakini ikiwa ni yeye ndiye ambaye anakuchukia, basi ni sawa kuchukua vile ulivyompa.

[1] al-Bukhaariy (5136), Muslim (1419) na Abu Daawuud (2092) na muundo ni wa kwake.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 468
  • Imechapishwa: 21/07/2025