Watoto wanakataa kutekeleza wasia wa mzazi wa Udhhiyah eti ni Bid´ah

Swali: Mwanaume mmoja amekufa na aliacha wasia wachinjiwe Udhhiyah wazazi wake. Lakini watoto wamekataa kwa kutoa hoja kwamba ni Bid´ah. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni wajibu kutekeleza wasia. Kama ameacha wasia juu ya wazazi wake utekelezwe. Achinjiwe yeye na wazazi wake, kama alivoacha anausia. Mtu amnuilie yeye na wazazi wake. Udhhiyah sio Bid´ah kwa mzazi wala wazazi wake. Bali ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa nia ya swadaqah. Maoni yanayosema kuwa ni Bid´ah ni kosa. Yamesemwa na baadhi ya watu na wamekosea. Udhhiyah ni Sunnah kwa waliohai na wafu wote wawili. Kwa hivyo ni wajibu kutekeleza wasia juu ya wasii na wazazi wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/13804/حكم-تنفيذ-وصية-من-اوصى-بالاضحية-عنه-وعن-والديه
  • Imechapishwa: 07/06/2024