Swali: Je, anapata dhambi yule ambaye anawaacha watoto zake wa kiume wenye umri wa miaka 13 na mfano wake wanaswali Fajr nyumbani mara nyingi?

Jibu: Ajitahidi kuwaamrisha kuswali msikitini, kuwapendeza nayo, kuwahimiza na kuandamana nao. Lakini afanye hivo kwa hekima. Siku ya kwanza aanze kwa swalah ya faradhi moja, siku nyingine faradhi mbili n.k. Ajaribu kadiri awezavyo wapende msikiti, kuandamanao nao na kuwafanyia upole.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-من-ترك-أبناءه-يصلون-في-البيت-دون-المسجد
  • Imechapishwa: 11/06/2022