Watoto wa chini ya miaka saba na safu ya kwanza

Swali: Baadhi ya watu wasiokuwa na elimu wamezowea kuwaondosha watoto katika safu ya kwanza. Wengine wameweka kikomo cha miaka na kusema kwamba wakiwa chini ya miaka saba basi hawana nafasi yoyote katika safu ya kwanza hata kama watakuja mapema.

Jibu: Ambaye yuko chini ya miaka saba aswali pamoja na familia yake. Hana swalah. Asiwaudhi watu na asiwatie uzito.

Swali: Akiingia na baba yake akitokea akazini?

Jibu: Haidhuru – Allaah akitaka – ikiwa ni kutokana na haja kama mfano wa kiti kinachokuwa kati yao au nguzo ya jengo inayokuwa katika safu.

Swali: Asogee mbele ya safu?

Jibu: Kinachokusudiwa ni kwamba azibe pengo kutokana na dharurah na kutokana na haja. Pengine amekuja naye kwa sababu hakuna wa kumwangalia huko alipo. Wakati mwingine anaweza kuhitajia na kulazimika jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23795/هل-يمنع-الصغار-من-الصف-الاول
  • Imechapishwa: 04/05/2024