Wasichana wa mama aliyeachika ni Maharimu kwa baba yao wa kambo?

Swali: Mama aliyetalikiwa akiolewa na akazaa watoto wa kike kwa yule mume wa pili. Je, inafaa kwa watoto wa kike hawa kupeana mikono na yule mume wa kwanza wa mama yao?

Jibu: Ndio, ni Maharimu. Mtu akimuoa mwanamke na kumjamii… ni lazima amwingilie kisha baadaye akamzalia watoto wa kike na baada ya hapo akamtaliki. Mwanamke huyo akaolewa na akazaa watoto wa kike, watoto wa kike hawa ni Maharimu kwa mwanamme huyo. Ni watoto wa kambo. Inafaa wakapeana mikono. Bora ni kumbusu shavuni, paji la uso na kwenye pua yake. Kufanya hivi ndio bora na si kwenye midomo.

Kuhusu akimuoa na akamtaliki kabla ya kumwingilia. Alifunga naye ndoa na hakuwahi kumjamii, wasichana hawa watakuwa ni wa kando na si Maharimu zake mume huyu wa kabla wala mume mwingine aliyekuja baada yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3803/%D9%87%D9%84-%D8%A8%D9%86%D8%A7%D8%AA-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B7%D9%84%D9%82%D8%A9-%D9%85%D8%AD%D8%A7%D8%B1%D9%85-%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%AC%D9%87%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AE%D8%B1
  • Imechapishwa: 19/05/2020