Swali: Je, mahari makubwa ni katika mambo kabla ya kuja Uislamu?
Jibu: Ndio. Ni katika mambo kabla ya kuja Uislamu ya sasa. Kwa sababu tumesema kuwa kila kinchoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah ni katika mambo kabla ya kuja Uislamu. Kwa hivyo miongoni mwa mambo kabla ya kuja Uislamu ya sasa ni kuchupa mipaka katika mahari. Hapa ni pale ambapo linamtia mume katika uzito. Lakini ikiwa mume ni muweza na akatoa milioni kwa khiyari yake, hapana vibaya kufanya hivo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَإِنْ أَرَدتُّمُ اسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا مِنْهُ شَيْئًا
“Na mkitaka kubadlisha mke mahali pa mke, na mmempa mmoja wao [zawadi ya] mirundi ya mali, basi msichukue humo chochote.”[1]
Kinacholengwa ni ´mirundi ya mali`. Ikiwa yuko vizuri na akapenda kutoa kwa kutaka kwake, hapana vibaya. Lakini kumwendea muislamu na kumtaka kwa mfano atoe 300.000 ili apate kuozeshwa ni katika mambo kabla ya kuja Uislamu. Huko ni kumfanyia vibaya mwanamke, na pia ni kumfanyia vibaya yule mposaji. Masikini huyu anamfanya msichana wake kama kondoo. Yeye haangalii iwapo mtu huyo ana uwezo kidini au kidunia. Pengine mwanaume ni chapombe akaja kumuua mke wake baada ya masiku kadhaa, kwa sababu ni chapombe. Kwa hiyo mahari makubwa ni kubaya juu ya dini, kubaya juu ya mwanamke na kubaya juu ya mposaji.
[1] 04:20
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 462
- Imechapishwa: 22/07/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket