Washauri wa mtawala wanatakiwa kuwa wanazuoni

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) anasema kuwa waliokuwa wakimkaza ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ilikuwa ni wanazuoni katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa ndio walikuwa wenye kumkaza; ni mamoja ikiwa ni wazee au vijana. Wanamshauri na kumwelekeza.

Vivyo hivyo inatakiwa kuwa kwa kila kiongozi wenye kumkaza wanatakiwa kuwa watu wema. Wanaomkaza ikiwa ni watu wasiokuwa wema, basi atapotea yeye na kuupoteza Ummah. Akikazwa na watu wema, Allaah atanufaisha Ummah kupitia wao. Kwa hivyo, ni wajibu kwa mtawala wenye kumkaza achague wanazuoni na watu wenye imani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/276)
  • Imechapishwa: 27/04/2023