Miongoni mwa faida ya Haiyth hii – Hadiyth ya Mu´aadh kutumwa Yemen – ni pamoja na kwamba Witr sio wajibu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuitaja. Ametaja tu swalah tano [kwamba ndio wajibu]. Haya ndio maoni yenye nguvu miongoni mwa maoni ya wanachuoni.

Wapo wanachuoni waliosema kuwa Witr ni wajibu.

Wengine wakafafanua zaidi na kusema yule ambaye ana mazowea ya kuswali na kusimama usiku, basi Witr kwake ni wajibu na yule asiyekuwa na mazowea basi sio wajibu.

Maoni sahihi ni kwamba sio wajibu kabisa. Kwa kuwa lau ingelikuwa wajibu basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angeliibainisha.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/504)
  • Imechapishwa: 23/09/2025