Wanazuoni kuhusu anayemtukana Allaah na Mtume wake

Swali: Kitabu ”al-Qawl al-Mufiyd” cha Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) anasema:

”Anayemtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haikubaliwi tawbah yake na ni wajibu kumuua, hilo ni tofauti na anayemtukana Allaah ambaye inakubaliwa tawbah yake na hauliwi. Haki yake inatofautiana na haki ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hilo ni kwa sababu Allaah ametueleza kuhusu haki Yake ya kwamba anasamehe madhambi yote kwa yule mwenye kumuomba msamaha, tofauti na kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Jibu: Wanazuoni wamekinzana juu ya suala hili. Ni moja ya maoni mawili:

1  – Tawbah ya mwenye kutukana inakubaliwa pale atapojutia na akaja hali ya kuwa ni mwenye kutubia. Tawbah yake inakubaliwa.

2 – Anauliwa, ni mamoja amemtukana Mtume au Allaah. Makinzano yanatambulika. Kilichotangaa kwa wanazuoni ni kwamba anayetukana tawbah yake haikubaliwi, anapaswa kuuliwa. Haki ya Allaah ndio kubwa zaidi. Hata hivyo makusudio yake ni pale inapokuja kuhusiana na kumtukana Mtume, kwa sababu hiyo ni haki ya kiumbe. Hayo ndio makusudio yake.

Swali: Je, anasimamishiwa adhabu ya Kishari´ah?

Jibu: Adhabu ni kuuliwa, hiyo ndiyo adhabu yake. Lakini akitujia hali ya kuwa ni mwenye kutubia na kujuta hatujamdhibiti. Sahihi ni kwamba anakubaliwa kama makafiri wengine waliosilimu baada ya kutukana.

Swali: Kwa hiyo hapewi udhuru kutokana na ujinga wake?

Jibu: Hapana, mtu hawi mjinga kwa mambo kama haya. Hata watoto si wajinga kwayo. Si wajinga kwamba kutukana ni dhambi. Huwezi kukuta mtoto anamtukana baba au kaka yake. Wanajua kuwa si jambo zuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24680/حكم-ساب-الله-تعالى-وساب-الرسول
  • Imechapishwa: 24/11/2024