Wanazungumzishwa waislamu wote kwa jumla

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fungeni kwa kuonekana kwake na fungueni kwa kuonekana kwake.”

Hapa wanazungumzishwa waislamu wote au kila watu wa nchi yao?

Jibu: Sahihi ni kwamba huu ni ujumbe kwa waislamu wote kwa ujumla. Hata hivyo baadhi ya wanazuoni wameona kwamba kila watu wa mji wana mwezi wao. Kwa hiyo hapana vibaya kwa maoni haya. Maoni haya yamekubaliwa na kundi la wanazuoni, akiwemo Ibn ´Abbaas na wengine. Lakini msingi katika maamrisho ya Shari´ah ni kuwa ni ya ujumla. Hili ndio msingi – kwamba maamrisho ya Allaah ndani ya Qur-aan na maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni ya ujumla kwa waislamu wote. Yeyote atakayekuja na hoja ya kuyafanya kuwa ya mji fulani tu, basi ni juu yake kuleta dalili ya kuonyesha hivyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25429/هل-حديث-صوموا-لرويته-لعموم-المسلمين-او-لاهل-كل-بلد
  • Imechapishwa: 01/04/2025