al-Ikhwaan al-Muslimuun wamefedheheka. Huanza kukuwaidhi watu na mwishoni husema.

“Kuweni wanachama wetu!”

Tunapaswa kuwalingania watu kwa ajili ya Allaah. Tunatakiwa kukubaliana na watu baadhi wasiwafuate kichwa mchunga wengine, asiwepo yeyote ambaye ataanzisha chama ambacho analingania kwacho na kwamba hakuna tunacholingania kwacho isipokuwa tu Qur-aan na Sunnah.

Hata hivyo sisi tuna mapungufu katika ulinganizi. Tunakiri jambo hilo. Tangu hapo kitambo nilikuwa nikisema hakujafanyika sehemu ya kumi ya yale yanayotakiwa kufanyika. Hivi sasa nasema kuwa sijafanya hata 2.5% ya yale yanayotakiwa kufanyika. Tuko wachache, uwezo wetu ni mdogo, lakini Mola anasema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Basi mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Laiti ulinganizi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun ungelifanywa kuwa huru ili waweze kushirikiana na ndugu zao Ahl-us-Sunnah. Haitakiwi kwao kuuza ulinganizi wao kwa mmisri, mukuwaiti au msaudi yeyote.

Nawashauri ndugu wawe wakweli kwa Allaah na wafanye matendo kikweli kwa ajili ya Allaah. Wasifanye kazi kwa ajili ya utawala wala kwa ajili ya mambo ya kidunia. Ni kwa nini wanawakataa ndugu zao Ahl-us-Sunnah na sambamba na hilo wanaenda kwa watenda madhambi, Suufiyyah, Shiy´ah na wengineo? Wanawaendea na kuwafungulia njia ili waweze kujiunga nao. Sambamba na hilo wanawatupilia mbali Ahl-us-Sunnah na kuwafanyia uadi. Hilo linafahamisha kutokufanywa kwa ajili ya Allaah.

[1] 64:16

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 336-337
  • Imechapishwa: 03/06/2025