Wanawake wenye hedhi wanaoenda misikitini wakati wa Tarawiyh

Swali: Baadhi ya wanawake wamezoea kuswali swalah ya Tarawiyh msikitini katika masiku ya Ramadhaan. Wanapojiliwa na hedhi wanasema kuwa wanataka kwenda na kuketi kandoni na msikiti ili kumfuatilia imamu na kujifunza kisomo sahihi. Je, inafaa kwake kufanya hivo?

Jibu: Ni sawa ikiwa yuko maeneo ambayo ni nje ya msikiti. Kwa mfano karibu na msikiti, nje ya msikiti. Hapana vibaya.

Swali: Katika chumba hichohicho cha wanawake?

Jibu: Ikiwa ni msikitini, hapana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24628/حكم-مكث-الحاىض-في-المصلى-لسماع-التراويح
  • Imechapishwa: 15/11/2024