Swali: Katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuna watu aina mbili wa Motoni sijawaona; wanaume walio na bakora kama mkia wa ng´ombe ambazo wanawapiga kwazo watu, na wanawake waliovaa vibaya, uchi, Maaylaat na Mumiylaat. Vichwa vyao ni kama nundu ya ngamia. Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake. Harufu yake inapatikana umbali wa kadhaa na kadhaa.”

Haya makemeo makali ni kwa yule tu ambaye kakusanya sifa zilizotajwa zote?

Jibu: Ni kwa yule aliyekusanya sifa zote hizi au baadhi yazo. Makemeo yanakusanya sifa zote na yanakusanya baadhi ya sifa hizi.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=qVPJq_oO-5U
  • Imechapishwa: 19/09/2020