Swali: Vipi ikikadiriwa wanaume wanasikia dufu la wanawake?
Jibu: Hata kama. Kupiga dufu ni Sunnah kwa wanawake. Hata hivyo haitakiwi kwao kunyanyua sauti sana.
Swali: Baadhi ya ndugu wanaposikia dufu wanakemea?
Jibu: Hapana. Muda wa kuwa ni kati ya wanawake haidhuru. Haijalishi kitu ikiwa watasikia walioko pambizoni na mlango. Huku ni kwa ajili ya kutangaza ndoa. Kutangaza ndoa hakukuwi isipokuwa kwa kufanya hivo. Vipi itakuwa kutangaza ikiwa hawasikii? Wasikie wanawake wenziwe.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23848/حكم-سماع-الرجال-دف-النساء-في-النكاح
- Imechapishwa: 18/05/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Wanawake wanaofanya kupiga dufu harusini ndio kazi ya pato lao
Swali: Ni ipi hukumu ya kuajiri wanawake kuja kupiga dufu? Jibu: Katika kazi za mkono si jambo zuri. Kupiga dufu katika mnasaba wa ndoa ni Sunnah kwa ajili ya kutangaza ndoa. Haitakikani mtu kufanya hii ndio kazi yake ya pato lake. Kutangaza Sunnah kunakusudiwa ndani yake mtu kupata ujira na hakukusudiwi…
In "Kazi ya mwanamke"
57. Hukumu ya wanawake kupiga dufu kwa ajili ya kutangaza ndoa
Imependekezwa kwa wanawake kupiga dufu ili ndoa itangazike na ienee na hayo yanafanyika kati ya wanawake peke yao. Dufu hilo lisiambatane na muziki, ala za pumbao wala sauti nzuri za wanawake. Katika mnasaba huu hakuna neno kwa wanawake kuimba mashairi kwa njia ya kwamba wasisikiwe na wanaume. Mtume (Swalla Allaahu…
In "09. Sura ya tisa: Hukumu zinazowahusu wanandoa"
Kupiga dufu bila ya kipaza sauti wala redio
Swali: Ni ipi hukumu ya kupiga dufu wakati wa harusi? Jibu: Haina neno. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) aliamrisha hilo. Aliamrisha wanawake kupiga dufu ili ndoa iweze kujulikana. Imependekezwa kwa wanawake kupiga dufu katika mazingira ya kike na wawe wao kwa wao. Hata hivyo haitakiwi kuimba kwenye kipaza sauti au…
In "Harusi"