Wanaopendana kwa ajili ya Allaah watakuwa katika ngazi moja?

Swali: Je, wale wanaopendana kwa ajili ya Allaah watakuwa na daraja sawa katika Pepo au watatofautiana?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) anasema:

”Wako wapi wanaopendana kwa ajili ya Utukufu Wangu? Hakika leo nitawatia kivulini katika kivuli Changu siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli Changu.”

Hadiyth nyingine inasema:

“Aina saba ambao Allaah atawatia kivulini katika kivuli Chake… ”

Miongoni mwao akataja wale wanaopendana kwa ajili ya Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29289/هل-تتفاوت-درجات-المتحابين-في-الله-في-الجنة
  • Imechapishwa: 31/05/2025