Swali: Baadhi ya watu wanatumia mbinu katika kulingania kwa namna ya kwamba wanalingania katika ubora wa matendo na wanaacha kulingania katika upwekeshaji kwa kusema eti inatenganisha baina ya watu.
Jibu: Hapana, hapana. Hili ni kosa. Ni katika ujinga wake. Kama anawalingania washirikina basi anatakiwa kuanza kwa upwekeshaji. Lakini kama anawalingania waislamu anatakiwa kuwakokoteza kuwa na msimamo katika haki na kumtii Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sambamba na hayo awatadharishe maasi, kwa sababu tayari wanamwabudu Allaah pekee. Lakini ikiwa anawalingania washirikina aanze kwa kuwalingania katika upwekeshaji na kuacha shirki. Hivo ndivo alivyoanza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawaamrisha Maswahabah kuanza nayo, kwa sababu shirki ndio dhambi kubwa mno.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24510/ما-حكم-زعم-ان-الدعوة-للتوحيد-تفرق-الناس
- Imechapishwa: 28/10/2024
Swali: Baadhi ya watu wanatumia mbinu katika kulingania kwa namna ya kwamba wanalingania katika ubora wa matendo na wanaacha kulingania katika upwekeshaji kwa kusema eti inatenganisha baina ya watu.
Jibu: Hapana, hapana. Hili ni kosa. Ni katika ujinga wake. Kama anawalingania washirikina basi anatakiwa kuanza kwa upwekeshaji. Lakini kama anawalingania waislamu anatakiwa kuwakokoteza kuwa na msimamo katika haki na kumtii Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sambamba na hayo awatadharishe maasi, kwa sababu tayari wanamwabudu Allaah pekee. Lakini ikiwa anawalingania washirikina aanze kwa kuwalingania katika upwekeshaji na kuacha shirki. Hivo ndivo alivyoanza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawaamrisha Maswahabah kuanza nayo, kwa sababu shirki ndio dhambi kubwa mno.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24510/ما-حكم-زعم-ان-الدعوة-للتوحيد-تفرق-الناس
Imechapishwa: 28/10/2024
https://firqatunnajia.com/wanalingania-katika-ubora-wa-matendo-na-kuacha-tawhiyd/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket