Wanajua Takfiyr lakini hawajui masuala yanayohusiana na twahara

Uliza kuhusu matamshi. Kuhusu watawala, usiwaulizie. Kwa sababu ima watahukumiwa kuwa ni makafiri au ni waislamu. Jambo hili wanaachiwa wanachuoni waliobebea katika elimu. Miongoni mwa makosa yaliyoenea kati ya vijana ni kwamba wao wenyewe wanajiona kuwa ni wenye kustahiki kukufurisha jambo ambalo ni gumu kabisa. Ukimuuliza mmoja wao masuala yanayohusiana na hedhi, anachanganyikiwa. Lakini inapokuja katika masuala yanayohusiana na kuhukumu ukafiri na kumtoa mtu nje na kumwingiza ndani ya Uislamu, utamuona ni mwenye ujasiri. Kumhukumu mtu mmoja mmoja sio kama kuweka msingi wa jambo fulani. Unapomuhukumu mtu mmoja mmoja basi unalazimika kuwauliza wanachuoni juu yake.

Kuhusu imani inayoisalimisha dini yako ambapo unakuwa ni mwenye kukufuru Twaaghuut na unajiweka mbali na yale yasiyomridhisha Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), huku ndio kusimika msingi. Kuhusu hukumu, haya ni masuala mengine. Hukumu inarejea kwa wanachuoni. Masualaa yanahitajia kuweka msingi. Kwa ajili hiyo utaona kuwa maneno ya wale wanachuoni waliobobea katika elimu yanayofautiana na maneno ya wale wenye kukurupuka. Hii ni kanuni muhimu kwa mwanafunzi. Mwanafunzi ni mwenye kujulikana kwa kujichunga kutokana na yale anayoyasema.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.maktabada.com/casharo_dagaal/Takfeer/takfeer-h.html
  • Imechapishwa: 22/03/2020