Wanafunzi wanatakiwa waende kuwalingania walioko vijijini

Swali: Unawanasihi nini wanafunzi katika ujio wao wa likizo hii khaswa katika uwanja wa kutafuta elimu na kulingania katika dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)?

Jibu: Nawanasihi kuhudhuria dawrah za kielimu zilizojaa. Ndani yake kuna faida na kheri. Vilevile wahudhurie mizunguko ya kielimu ambayo watafaidika kwayo. Wafaidike na yale yaliyorekodiwa katika kanda. Wawatembelee wanachuoni. Wasome katika vitabu vyenye faida. Wasimame na jukumu la kulingania. Wawatembelee ndugu. Kufanya utafiti pamoja na wanachuoni na wanafunzi katika yale mambo yanayotatiza.

Kuhusu uwanja wa kulingania nawashauri wawasiliane na wanafunzi walioko katika kitengo cha Da´wah kwa ajili ya kwenda kuwatembelea walioko vijijini, kuwapa faida na kuwafunza. Wengi walioko vijijini hawajui namna ya kuswali na wala hawajui al-Faatihah. Ndugu wakiwatembelea, wakawafunza na wakawaelekeza basi ndani yake kuna kheri. Kwa sababu yule mwenye kulingania katika kheri ni kama aliyeifanya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 08/03/2019