Wanafunzi kutumia fursa pindi mahujaji wanapoenda Makkah

Swali: Tulikuwa tunaomba uwape kalima ndugu zetu wanafunzi kuhusu kutumia fursa ya wakati huu wa hajj katika kulingania kwa Allaah na kuwaelekeza waislamu katika ´Aqiydah sahihi?

Jibu: Hili ni wajibu kwa wanafunzi. Hapana shaka kwamba ni fursa kubwa. Kwani watu wamekusanyika kutoka katika kila pembe ya dunia na hivyo awalinganie kwa Allaah kwa kuwaamrisha mema, kuwakataza maovu na awawekee wazi ´Aqiydah ya Salafiyyah ambayo ndio sahihi na wakati huohuo kuwakataza Bid´ah. Huu ndio wajibu kwa wanafunzi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 06/01/2019