Swali: Kundi la watu walikuwa nje ya mji wa Riyaadh katika sehemu ya mapumziko. Karibu nao kulikuwa na msikiti uliokuwa umbali wa takriban 500 km. Wakaswali katika sehemu hiyo ya mapumziko kwa kukhofia kutawanyika kwao. Ni ipi hukumu ya swalah yao?
Jibu: Hapana neno ikiwa msikiti uko mbali na hawasikii adhaana kwa sauti ya kawaida. Ama ikiwa wanasikia adhaana kwa sauti ya kawaida, basi ni wajibu kwao kumuitikia mwenye kuita. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote mwenye kusikia wito kisha asiitikie, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.” Ibn ´Abbaas akaulizwa: ”Udhuru ni nini?” Akasema: ”Ni khofu au ugonjwa.”
Lau wangeenda msikitini, basi ingekuwa bora zaidi, hata kama ni kwa gari. Lakini ikiwa waliswali kwa nia hiyo, kwa maana kwa kukhofia kutawanyika kwao, basi wana mashiko, ingawa lililo bora ni kuswali msikitini.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
- Imechapishwa: 24/09/2026
Swali: Kundi la watu walikuwa nje ya mji wa Riyaadh katika sehemu ya mapumziko. Karibu nao kulikuwa na msikiti uliokuwa umbali wa takriban 500 km. Wakaswali katika sehemu hiyo ya mapumziko kwa kukhofia kutawanyika kwao. Ni ipi hukumu ya swalah yao?
Jibu: Hapana neno ikiwa msikiti uko mbali na hawasikii adhaana kwa sauti ya kawaida. Ama ikiwa wanasikia adhaana kwa sauti ya kawaida, basi ni wajibu kwao kumuitikia mwenye kuita. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote mwenye kusikia wito kisha asiitikie, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.” Ibn ´Abbaas akaulizwa: ”Udhuru ni nini?” Akasema: ”Ni khofu au ugonjwa.”
Lau wangeenda msikitini, basi ingekuwa bora zaidi, hata kama ni kwa gari. Lakini ikiwa waliswali kwa nia hiyo, kwa maana kwa kukhofia kutawanyika kwao, basi wana mashiko, ingawa lililo bora ni kuswali msikitini.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
Imechapishwa: 24/09/2026
https://firqatunnajia.com/wana-pikniki-wanaacha-kwenda-kuswali-msikitini-uliyo-karibu-nao/