Mashindano ya kibiashara ambayo ni sharti ununue bidhaa

Swali: Ni ipi hukumu ya mashindano ya kibiashara yanayowekwa madukani, ambapo wanaweka sharti la kununua bidhaa ili mtu aweze kuingia katika mashindano?

Jibu: Mashindano haya hayaruhusiwi. Isitoshe ni katika kamari. Ikiwa mashindano yatawekewa sharti la kununua, basi hayaruhusiwi, hata kama ni gazeti. Kwa sababu kila mmoja akinunua gazeti kwa pesa moja au pesa mbili, wao hukusanya maelfu na mamilioni, kisha hutoa sehemu ndogo tu ya fedha walizozikusanya kama zawadi. Ama ikiwa ni mashindano ambayo mtu halipi chochote wala hanunui kitu chochote ili kushiriki, basi hakuna tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 24/09/2026