ar-Raajihiy kuhusu kuswali Rak´ah nne kwa pamoja kwa salamu moja

Swali: Je, inajuzu kuunganisha Sunnah mbili za kabla ya Dhuhr zikawa Rak´ah nne mfululizo?

Jibu: Sunnah ni kutoa salamu baada ya kila Rak´ah mbili. Ahnaaf wanaziswali kwa salamu moja. Hadiyth inasema:

”Swalah ya usiku ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Imekuja katika riwaya ya an-Nasaa’iy:

”Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Hata hivyo baadhi ya wanazuoni wameidhoofisha sentesi isemayo “… na mchana”.

Kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kwamba hapana neno kuswali Rak´ah nne kwa salamu moja wakati wa mchana. Lakini lililo bora ni kutoa salamu baada ya kila Rak´ah mbili. Ama usiku haijuzu kutoa salamu baada ya zaidi ya Rak´ah mbili, isipokuwa ikiwa amenuia kuziswali kuwa Witr. Kwa hiyo anaswali Witr ya Rak´ah tatu, tano, saba au tisa. Ama kuswali Rak´ah nne kwa salamu moja au Rak´ah sita kwa salamu moja, hili halijuzu. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh:

”Swalah ya usiku ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Hii ina maana ya amri. Kwa maana nyingine Hadiyth inasema:

“Swaslini usiku [Rak´ah] mbilimbili.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 24/09/2026