Kukusanya Sunnah ya Maghrib pamoja na Sunnah ya ´Ishaa

Swali: Ni ipi hukumu ya kukusanya Sunnah ya Maghrib ambayo inakidhiwa pamoja na Sunnah ya swalah ya ´Ishaa?

Jibu: Hakukusanywi Sunnah mbili, bali kila Sunnah inaswaliwa peke yake. Wakati wa ´Ishaa unapoingia basi Sunnah ya Maghrib muda wake huwa umepita. Yenyewe hukidhiwa ndani ya wakati wake. Isipokuwa Sunnah ya Fajr; mtu ana uchaguzi wa kuikidhi baada ya swalah au baada ya kuchomoza kwa jua. Ama Sunnah nyingine, hukidhiwa ndani ya wakati wake. Sunnah ya Dhuhr ya kabla na baada yake, wakati wake unaendelea mpaka wakati wa ´Aswr unapoingia. Sunnah ya Maghrib, wakati wake unaendelea mpaka adhaana ya ´Ishaa. Sunnah ya ´Ishaa wakati wake unaendelea mpaka nusu ya usiku.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 24/09/2026