Swali: Ni ipi hukumu ya kutekeleza swalah ya kuomba mvua shuleni? Na wakati wake huanza lini?
Jibu: Swalah ya kuomba mvua haitekelezwi shuleni, bali hufanywa katika viwanja kwa mujibu wa utaratibu wa alivyopanga mtawala. Isipokuwa ikiwa kuna tangazo kutoka Wizara kuwa iswaliwi shuleni, basi hilo ni jambo jingine. Inawapasa waislamu kuipa umuhimu swalah ya kuomba mvua na kutopuuza Sunnah. Baadhi yao huipuuza na kulala, jambo ambalo ni kosa. Bali inampasa mtu kushiriki pamoja na waislamu katika swalah na du´aa yao. Huenda rehema ikateremka na ikamfikia pamoja nao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
- Imechapishwa: 24/09/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kutekeleza swalah ya kuomba mvua shuleni? Na wakati wake huanza lini?
Jibu: Swalah ya kuomba mvua haitekelezwi shuleni, bali hufanywa katika viwanja kwa mujibu wa utaratibu wa alivyopanga mtawala. Isipokuwa ikiwa kuna tangazo kutoka Wizara kuwa iswaliwi shuleni, basi hilo ni jambo jingine. Inawapasa waislamu kuipa umuhimu swalah ya kuomba mvua na kutopuuza Sunnah. Baadhi yao huipuuza na kulala, jambo ambalo ni kosa. Bali inampasa mtu kushiriki pamoja na waislamu katika swalah na du´aa yao. Huenda rehema ikateremka na ikamfikia pamoja nao.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
Imechapishwa: 24/09/2026
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-kuomba-mvua-shuleni/