Swali: Ni ipi hukumu ya kusema uongo ikiwa ni uongo mdogo tu, kama vile kumdanganya mtu ili nisipoteze urafiki wake?
Jibu: Umm Kulthuum bint ´Uqbah ibn Abiy Mu´iytw (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema
”Sikumsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiruhusu uongo katika jambo lolote isipokuwa katika mambo matatu: katika kupatanisha watu, katika vita na katika maneno ya mume kwa mkewe na mke kwa mumewe.”
Haya ndiyo yaliyobaguliwa.
Kwa hiyo kupatanisha watu, katika vita – kwani vita ni hila – na baina ya mume na mke ambapo anaweza kumwambia maneno ambayo si ya kweli kabisa kwa ajili ya kurekebisha hali yao na kuimarisha maisha yao ya ndoa bila kumdhuru yeyote. Haya ndiyo mambo aliyoyaruhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika uongo. Ama yasiyokuwa haya matatu, basi ni lazima kujiepusha na uongo na kuuhadhari. Mtu ajizoeshe kusema kweli katika maneno yake na matendo yake na iwe ndiyo tabia yake ya kudumu. Isipokuwa ikiwa kusema kweli kutaleta madhara au kusababisha fitina, basi hilo lina hukumu yake maalum. Mfano ikiwa dhalimu anamuulizia mtu ili amuue au amdhulumu, basi hairuhusiwi kusema kweli kwa kumwonyesha alipo, bali atasema kuwa hajui hata kama anajua ili kulinda nafsi ya yule anayelengwa.
Kadhalika anayepatanisha watu, anasema maneno mazuri au ananukuu mema ili kuleta suluhu.
Kwa kumalizia uongo unaruhusiwa katika mambo haya matatu na pia pale ambapo Shari´ah imefahamisha kufaa kwa ajili ya kuwalinda waislamu dhidi ya madhara, maadui au dhuluma na mfano wa hayo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3352/خطورة-التهاون-في-الكذب
- Imechapishwa: 23/09/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kusema uongo ikiwa ni uongo mdogo tu, kama vile kumdanganya mtu ili nisipoteze urafiki wake?
Jibu: Umm Kulthuum bint ´Uqbah ibn Abiy Mu´iytw (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema
”Sikumsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiruhusu uongo katika jambo lolote isipokuwa katika mambo matatu: katika kupatanisha watu, katika vita na katika maneno ya mume kwa mkewe na mke kwa mumewe.”
Haya ndiyo yaliyobaguliwa.
Kwa hiyo kupatanisha watu, katika vita – kwani vita ni hila – na baina ya mume na mke ambapo anaweza kumwambia maneno ambayo si ya kweli kabisa kwa ajili ya kurekebisha hali yao na kuimarisha maisha yao ya ndoa bila kumdhuru yeyote. Haya ndiyo mambo aliyoyaruhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika uongo. Ama yasiyokuwa haya matatu, basi ni lazima kujiepusha na uongo na kuuhadhari. Mtu ajizoeshe kusema kweli katika maneno yake na matendo yake na iwe ndiyo tabia yake ya kudumu. Isipokuwa ikiwa kusema kweli kutaleta madhara au kusababisha fitina, basi hilo lina hukumu yake maalum. Mfano ikiwa dhalimu anamuulizia mtu ili amuue au amdhulumu, basi hairuhusiwi kusema kweli kwa kumwonyesha alipo, bali atasema kuwa hajui hata kama anajua ili kulinda nafsi ya yule anayelengwa.
Kadhalika anayepatanisha watu, anasema maneno mazuri au ananukuu mema ili kuleta suluhu.
Kwa kumalizia uongo unaruhusiwa katika mambo haya matatu na pia pale ambapo Shari´ah imefahamisha kufaa kwa ajili ya kuwalinda waislamu dhidi ya madhara, maadui au dhuluma na mfano wa hayo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3352/خطورة-التهاون-في-الكذب
Imechapishwa: 23/09/2026
https://firqatunnajia.com/uongo-mdogo-au-mwepesi/