Swali: Ni ipi tafsiri ya maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا

“Wale ambao wanatimiza nadhiri zao na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea.”[1]?

Jibu: Hii ni nadhiri ya utiifu iliyotajwa na Allaah pasi na kutundika na kukusudia. Bali tmu amemuwekea Allaah nadhiri na akajikurubisha kwayo Kwake kwa njia inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yetote mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Allaah, basi na amtii.”

Hata hivyo wamekatazwa kuianza. Lakini akishaiweka basi ni lazima aitekeleze muda wa kuwa ni nadhiri ya kumtii Allaah (Jalla wa ´Alaa).

[1] 76:07

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24394/ما-تفسير-قوله-تعالى-يوفون-بالنذر
  • Imechapishwa: 05/10/2024